
1. Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.
2. Changanya vizuri isiwe na madonge.
3. Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.
4. Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.
5. Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta.
6. Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili
7. Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.
8. Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cacao vijiko viwili vidogo vya chai. Inapochanganyika cacao vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cacao.
(cacao ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.