
habari za kazi chief,
ninafurahishwa na kupendezwa na kazi zako za kuakikisha kila mtu anaanda/kupika chakula kinavyotakiwa na kupata ladha nzuri.
Ila mi kwenye hii subject ya maandalizi ya CHAPATI, umenichanganya kwenye hicho kipimo cha Kikombe kidogo cha chai, mi nimeshindwa kuelewa kikombe kidogo cha chai ni kipi, maana siku hizi kuna kila aina ya vikombe.
Ningeomba uwe unaweka vipimo kwenye UNITS, pamoja na hivyo vya kukadiria kama kikombe cha chai n.k, maana si wote tunauwezo wa kuwa na hivyo vipimo vya Units.
Nakutakia kazi njema Chief Issa
Mimi kukanda chapati wakati mwingine huwa natumia maji ya baridi ambayo nimeyatoa kwenye friji, yaani yabaridi sana tuseme ninayaweka kwenye friza kabla hayajaganda ndio nakandia chapati. Kisha unga ukishakandika, nakata ukunja vidonge navisukuma kisha napaka samli kidogo au ghee au mafuta yoyote kidogo sana kisha naukunja tena kuwa vidonge vidogo vidogo. Nikishamaliza kukunja wote, ndio naanza sasa kusukuma chapati zangu na kuzichoma. Kwa kuwa tayari unga una mafuta natumia mafuta kidogo sana kuchomea.
Hizo cgapati zinaweza kukaa hata siku 2 au 3 bado laini zinalika bila wasi2
NB: Wakati mwingine naweka viazi au vitunguu kwenye huo unga kuongeza ladha.
Kaka Issa nashukuru sana kwa haya mapishi ya chapati na maandazi,upishi wangu sio mzuri chapati zangu huwa ngumu kama ubao hata kuzikunja wakati wa kula haziwezekani, nilikuwa nimepanga kukuuliza kama utatuwekea hii subject. Nimefurahishwa sana na wepesi wa mapishi yako ni lazima niyafanyie kazi siku za hivi karibuni. Je waweza kutuandikia na mapishi ya sambusa? -MDAU, USA
mimi nimekula chapati lakini chapati zetu za atl za dada Linda ni tamu jamani chapati kama croissant! embu aulizwe zinapikwaje jamani mh yule dada mashalau anapika chapati hata wa Iran hawaingii sijui wahindi waharabu ziro! tena mimi uwa nazila na chai sitaki mchuzi wala maharagwe mana ntaharibu radha,chapati za Linda express mwishoooo!
yaan bro huwa tunabishana sana kwenye kupika chapati kila mtu anaweka kipimo chake thankfully unaweka na kiasi cha kipimo jaman..
very hapi maana moja ya hobbies zangu ni kupika.
thanx a great deal.
mie nakaa mbali na nyumbani and also have been dying to understand how make chapatis.
Mimi naona chef Issa yupo sahihi.Unajua asilimia kubwa ya sis tuliokulia huku kwetu tz anatusaidia sana.
Maana ukiniambia unit sijui mililita kwa kweli utatupoteza wengi na wachache ndio watao mpata.Hususani tukiwa tunatengeneza maakuli ya nyumbani.
ILA kama ndio kutengeneza misosi ya magharibu au asia ya mbali sio mbaya akiweka hivyo vipimo vyenu vya unit au moto sio 200-250 dakika 10-15
ila kwa issue ya chapati,makande wali biriani nafikiri bado anaweza kutumia vipimo asilia.
kila la kheri chef
HABARI ZANGU ZAIDI
Issa Kesu Dar es salaam, Tanzania As Chef into with excellent qualification along with a strong need to stand out within this professional in Hazard Analysis and demanding control points (HACCP) which enable me to show my dedication to food safety and client satisfaction, in addition to continuously meeting the expectations of the altering world. The scope of my experience includes food production in cold kitchen, Pastry, Banqueting, A la carte, staff training and carving. View my complete profile